Psalms 121

Bwana Mlinzi Wetu

Wimbo wa kwenda juu.

1Nayainua macho yangu nitazame vilima,
msaada wangu utatoka wapi?
2 aMsaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.

3 bHatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia,
4 chakika, yeye alindaye Israeli
hatasinzia wala hatalala usingizi.
5 d Bwana anakulinda,
Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
6 ejua halitakudhuru mchana,
wala mwezi wakati wa usiku.
7 f Bwana atakukinga na madhara yote,
atayalinda maisha yako,
8 g Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,
tangu sasa na hata milele.
Copyright information for SwhNEN